🇹🇿 How Ouroboros Leios will change the Cardano Consensus

Source https://forum.cardano.org/t/how-ouroboros-leios-will-change-the-cardano-consensus/105836/1
Cardano hutumia makubaliano ya PoS, ambayo wakati wa kuandika ina uwezo wa kushughulikia shughuli 300 kwa sekunde moja. Hiyo ni karibu mara 50 zaidi ya makubaliano ya PoW ambayo Bitcoin hutumia. Walakini, kwa mfumo wa kifedha wa kimataifa, hii bado haitoshi. Timu ya IOG inafanyia kazi toleo jipya la PoS ambalo wamelipa jina la Ouroboros Leios.

Trilemma ya Blockchain
Timu ya wasanidi/kutengeneza mtandao wa blockchain husawazisha sifa tatu muhimu, ambazo ni usalama, ugatuaji na upanuzi. Trilemma ya blockchain
inarejelea imani iliyoenea kwamba mitandao iliyogatuliwa inaweza tu kutoa faida mbili kati ya tatu kwa wakati wowote. Usalama ni kipengele kisicho na masharti ambacho hakiwezi kuathiriwa. Timu husawazisha kati ya ugatuaji na upanuzi. Hata hivyo, kupendelea upunguzaji wa nafasi badala ya ugatuaji sio suluhisho bora, kwani ugatuaji ni kipengele muhimu cha tasnia ya blockchain. Zaidi ya hayo, jinsi ugatuaji unavyopungua, mgawo wa Nakamoto hupungua vile vile usalama hupungua

Kuunda mtandao wa blockchain ambao unafikia kiwango cha juu cha uwezo bila kuonyesha ukuwaji kipindi matumizi yanaongezeka na hautoi uwezo wa kufanya kazi bila kupitia mamlaka au mtu kati ikiwa usalama bado ni changamoto ya kiteknolojia kwa tasnia ya blockchain hilo nitatizo.

Cardano kwa sasa ni mojawapo ya mitandao iliyogatuliwa zaidi, ikiwa na zaidi ya waendeshaji elfu moja wanaozalisha Pools .Ni muhimu kwamba Cardano idumishe ugatuaji wake wa sasa wa madaraka na haifungi mlango wa ukuaji zaidi. Walakini, kuongezeka kwa uzani pia ni muhimu kwa misheni ambayo Cardano inajaribu kutimiza.

Ouroboros Leios ni kiendelezi kikuu kwa makubaliano ya sasa ya PoS ambayo yataongeza kwa kiasi kikubwa kiwango cha ugatuaji na kudumisha kiwango cha sasa cha ugatuaji. Hebu tuangalie maelezo yanayojulikana hadi sasa.

Usafirishaji wa data
Mitandao ya Blockchain hutumia blocks kwa kukusanyia miamala na scripts ambapo makubaliano ya mtandao hutokea. Kwa mtazamo wa mtandao, si vyema kufanya maamuzi katika ngazi ya kimataifa kwa kila shughuli ya mtu binafsi. Ni vyema zaidi kuchukua miamala mingi kwa wakati mmoja na kufanya uamuzi (makubaliano) juu ya mkusanyiko mzima.

Block ni mahali katika blockchain ambapo habari huhifadhiwa na kusimbwa

Iwapo wengi wa mtandao watazingatia block uliopendekezwa kuwa halali iliyo thibitishwa, Block mpya itahifadhiwa kwenye blockchain kwa kipindi chote na hapa ndio inakuwa mwanzo wa kutengeneza block ingine kwa ajili ya kuhalalishwa au kupitishwa na kujiunga kwa blockchain.

Vigezo viwili vinaathiri makadirio ya shughuli zinazofanywa na mitandao ya blockchain katika muda ulio wekwa,ambyo ni ukubwa wa block na muda wa block kukamilisha miamala iliyo halalishwa au kupitishwa

Ukubwa wa block hufafanua ukubwa wa juu wa Block, ambayo huathiri idadi ya miamala na scripts zinazoweza kutoshea ndani yake. Ikiwa ukubwa wa block ni 88 kB (90.112 B) na shughuli rahisi ina ukubwa, sema 300 B, miamala 300 inaweza kutoshea kwenye block.

Muda wa block hufafanua muda kati ya kuongeza block mpya. Cardano ina muda wa block umewekwa kuwa sekunde 20. Hii ina maana kwamba katika dakika 1 Cardano inaweza kufanya miamala 900 . Katika dakika 10, miamala 9000, nk.

Inaweza kutokea kwamba ikiwa idadi ya watumiaji ambao wanataka kutumia mtandao huanza kukua, mtandao hauwezi kuingiza shughuli zote mpya kwenye block mpya. Hivyo, baadhi ya shughuli lazima kusubiri katika mem-pool kwa block inayofwata

Kwa mfano, hii ingefanyika ikiwa watumiaji 400 wangetaka kutuma muamala rahisi ndani ya sekunde 20, na hii ingerudiwa kwa saa moja. Shughuli 400 ni zaidi ya 300 ambazo Cardano inaweza kushughulikia kwa urahisi. Kila baada ya sekunde 20, miamala 100 huachwa nje ya block , kwa hivyo lazima ibaki kwenye kundi la mem pool.

Unaweza kufikiria mem-pool kama hazina ya muda ya shughuli kwenye node za mtandao. Mhidhinishaji wa block anakuwa kiongozi wa yanayopangwa, yaani, anapata haki ya kuunda block mpya ,Block iliyo idhinishwa inachukua miamala iliyoidhinishwa awali kutoka kwa mem-pool na kuziweka kwenye Block. Kisha hueneza au kusambaza block kwenye mtandao. Kwa kila block mpya iliyoongezwa husambazwa kwa kila node .Pia nafasi ya mem-pool huongezeka kwani miamala ambayo tayari iko kwenye blockchain inaweza kutolewa kwa Mem pool. Kwani shughuli mpya zinakuja kila wakati Mem pool inatakiwa iwe na nafasi ya kupokea miamala mipya.

Ikiwa idadi ya miamala ni ya juu mara kwa mara kuliko nambari ambayo mtandao unaweza kushughulikia, ni muhimu kuzuia mem-pool kujaza zaidi ya kikomo kinachohitajika. Mtandao unalazimika kukataa shughuli mpya. Watumiaji lazima wasubiri kwa muda mrefu zaidi kwa ajili ya utatuzi wa miamala ambayo tayari iko kwenye kundi la mem pool. Watumiaji ambao wameshindwa kuwasilisha muamala lazima wajaribu tena. Watumiaji wanatarajia kuwa sulihisho litakuwa la muda mfupi na mtandao hautakuwa na matatizo ya uhalalishaji wa miamala iliyopitishwa kwa ajili ya blockchain.

Mem-pool ina uwezo wa kuchukua miamala kwa muda mfupi, lakini haina maana kwa kuwa na uwezo mkubwa kuliko ukubwa wa block. Iwapo kungekuwa na miamala ya kutosha kwenye hifadhi ya mem pool , tuseme, pool 100 zaidi, itamaanisha kwamba miamala mpya iliyowasilishwa haitaingia kwenye block kwa muda mrefu. Kwa hakika, hifadhi ya kumbukumbu inapaswa kuwa ndogo iwezekanavyo na mtandao unapaswa kuongezeka vya kutosha ili shughuli zisikae kwenye hifadhi ya mem pool kwa sababu tu hazitoshelezi kwenye block.

Mtandao ambayo iko decentralised inaweza kueneza miamala kwa haraka na unazuiliwa na kipimo data cha mtandao. Mtandao ya kawaida ina matokeo ya juu kuliko mitandao ya blockchain kwani blockchains hupunguzwa na ukubwa wa block na muda block inavyo dhibitishwa. Kwa maneno mengine, mitandao ya blockchain kwa sasa haiwezi kuwa na mtandao wa kutosha linapokuja suala la utengenezaji wa pool. Kinachorudisha nyuma mitandao ya blockchain ni makubaliano ya polepole ambayo pia yanadhibitiwa na saizi ya data katika muda fulani. Ingawa shughuli zinaweza kutiririka kupitia mtandao wa blockchain kwa haraka, Ila matokeo pekee ni kwamba mem-pool itajaa

Kuna utatuzi wa rahisi kama vile kuongeza ukubwa wa block au kupunguza muda wa block. Zote mbili husababisha matokeo ya juu zaidi kwani miamala mingi ingetoshea kwenye block na block mpya zingetengenezwa mara kwa mara. Kwa bahati mbaya, kubadilisha vigezo hivi kunaweza kuwa na athari mbaya kwa usalama na decentralisation. Kwa mfano, kadiri block inavyokuwa kubwa, ndivyo inavyochukua muda mrefu kueneza katika mtandao (kuongezeka kwa ucheleweshaji). Kadiri saizi ya block inakuwa ndogo, ndivyo uwezekano wa kuuunda fork kujitokeza, kwani utayarishaji wa block unaweza usipokee block ya mwisho kwa wakati na kutumia block iliyotangulia.

Kadiri idadi ya node kwenye mtandao inavyoongezeka, idadi ya sehemu ambayo data inapaswa kupita kwenye mtandao inaongezeka. Kila node inapothibitisha data kabla ya kuituma (ili kuzuia kutuma data isiyo sahihi kwenye mtandao), usambazaji wa data hupungua.

Note:
Proof of Stake (POS) ni aina ya utaratibu wa makubaliano unaotumiwa
kuthibitisha miamala ya cryptocurrency. Kwa mfumo
huu, wamiliki wa cryptocurrency wanaweza kuweka
sarafu zao, ambayo inawapa haki ya kuthibithisha
block mpya na kuziongeza kwenye blockchain

Proof of Work (POW) ni aina ya kuongeza block mpya za miamala kwenye
blockchain ya cryptocurrency.Kazi katika shughuli hii,
inazalisha hash (msururu mrefu wa herufi)
unaolingana na hash ya block ya mwanzo. Minner wa
crypto anayefanya haya mahesabu anapata haki ya
kuongeza block hyo kwenye blockchain na kupokea
tuzo.

Nodes ni moja ya kompyuta zinazoendesha programu ya blockchain ili
kuhalalisha na kuhifadhi historia kamili ya miamala kwenye
mtandao

Block ni miundo ya data ndani ya hifadhidata ya blockchain, ambapo data
ya muamala katika blockchain ya cryptocurrency inarekodiwa kwa
muda wote hubaki kwenye blockchain bila kuweza kufanyiwa
mabadiliko yoyote.

Mempool Ni aina ya chumba cha kungojea kwa miamala inayosubiri ya
sarafu ya crypto. Kama ilivyoelezwa hapo awali, miamala ya
crypto haifanywi na kukamilishwa kwa wakati mmoja. Badala yake, l azima zidhibitishwe na mtandao wa blockchain wa nodi ili
kuchakatwa. Hili linaweza kuchukua muda, kwa hivyo muamala
unaosubiri unahitaji mahali pa kufikia wakati unangoja uthibitishaji.
Hii “mahali fulani” ni mempool.

Blockchain ni daftari la pamoja, lisiloweza kubadilika ambalo huwezesha mchakato
wa kurekodi miamala na kufuatilia mali katika mtandao wa biashara.

Blockchain Trillema Hii ina maana kwamba kwamba mitandao iliyogatuliwa inaweza
tu kutoa faida mbili kati ya tatu kwa wakati wowote kuhusiana na
ugatuaji, usalama na upanuzi.

Decentralisation maana yake ni Ugatuaji au tunaweza sema ni uhamisho wa
udhibiti wa shughuli au shirika kwa ofisi kadhaa za mitaa na
kupewa mamlaka ya juu ya kuamua jambo fulani badala ya kuwa
na mamlaka moja.

1 Like