Cardano Digest kwa Kiswahili — 30 Septemba 2026 | Miaka 9 ya Cardano, CIP-113, Node 11.1.3 na TOKEN2049 Singapore

Karibu kwenye Cardano Community Digest!

Timu ya jamii ya Cardano Foundation inatoa Digest hii kila baada ya wiki mbili, ili kuwaletea habari, updates na matukio kuhusu Cardano na ekosistemi yake.

Kama unapenda kupokea Community Digest moja kwa moja kupitia email, unaweza kujiandikisha. :link: Hapa

Katika toleo hili

  • Miaka 9 ya Cardano: Miaka tisa tangu block ya kwanza, stake pools 2,890, miamala milioni 123.98 na hatua 158 za utawala.

  • CIP-113: Kiwango cha programmable token-like assets kimeingizwa kwenye hazina kuu ya CIP.

  • Cardano Node 11.1.3: Update inayorekebisha tatizo la kusoma anwani za IPv4, bila kuhitaji ledger replay.

  • TOKEN2049 Singapore: Stand ya Cardano Foundation ya mita za mraba 108, miradi 20 na shughuli mbalimbali tarehe 7–8 Oktoba.

  • Developer Spotlight: Maximilian Weber anaeleza namna ODATANO na OData zinavyorahisisha kuunganisha Cardano na mifumo ya biashara.

  • Updates za CIP: Mapendekezo sita mapya na kukamilika kwa CIP-113.

  • Habari za ekosistemi: Midnight, Cardano DeFi na kazi za waundaji wa maudhui.

  • Mafunzo kwa jamii: Subbit.xyz, malipo ya usajili na usalama wa smart contracts wakati wa maendeleo ya AI.

  • Cardano Foundation na Intersect: Ushirikiano na UCLA, Barça Fan Lab, x402, matokeo ya uchaguzi wa Board na maandalizi ya Dijkstra.

Habari hizi na nyingine nyingi ziko katika Digest ya leo.


:birthday_cake: Miaka 9 ya Cardano!

Tarehe 23 Septemba ilitimiza miaka tisa tangu kuundwa kwa block ya kwanza ya Cardano, inayojulikana kama genesis block. Tangu hapo, mtandao umepitia vipindi vitano: Byron, Shelley, Goguen, Basho na Voltaire.

Kila kipindi kimeleta hatua kubwa katika maendeleo ya mtandao: kuanzia uzinduzi wa Byron mwezi Septemba 2017, ugatuaji kupitia Shelley mwezi Julai 2020, smart contracts kupitia Goguen, kazi ya Basho ya kuongeza uwezo wa mtandao, hadi Voltaire, ambayo inaleta utawala unaoongozwa na jamii. :link: Maelezo ya vipindi vya Cardano na hard forks

Safari ya utawala nayo imepitia hatua nyingi. Ilianzia kwenye mfumo wa CIP-1694 na warsha za Katiba zilizofanyika duniani, ikafika kwenye mkutano wa kwanza wa Katiba huko Buenos Aires na Nairobi mwezi Desemba 2024, ambapo wajumbe waliidhinisha rasimu ya Katiba.

Baadaye, mchakato uliendelea kwenye blockchain, na jamii ya Cardano ikapitisha Katiba mwezi Februari 2025.

Katika taarifa yake ya tarehe 23 Septemba, Cardano Foundation ilihesabu:

  • Stake pools 2,890;

  • Blocks milioni 13.98;

  • Miamala milioni 123.98;

  • Kura 36,322 kwenye hatua 158 za utawala.

Baada ya miaka tisa, Cardano imeendelea kutoka kwenye kujenga mtandao hadi kujenga mifumo inayowezesha jamii yake kuutawala.:link:Fuata video Kamili hapa

:gear: CIP-113 Programmable Tokens imeingizwa kwenye hazina kuu ya CIP

Baada ya miaka ya kazi na ukaguzi, kiwango cha CIP-113 kimeingizwa kwenye hazina kuu ya Cardano CIPs tarehe 29 Septemba. Hii ni hatua muhimu kuelekea matumizi ya programmable tokens kwenye Cardano.

Kiwango hiki kinatoa mfumo wa mali zinazoweza kubeba sheria kama:

  • Orodha za watu wanaoruhusiwa baada ya KYC;

  • Orodha za watu wanaozuiwa;

  • Kufungia mali;

  • Kuweka mipaka ya uhamisho;

  • Masharti yanayohusiana na sheria za nchi au maeneo fulani.

Sheria hizo hutekelezwa kwenye blockchain kila wakati mali inapohamishwa. Hii inaweza kuwa muhimu hasa kwa mali zilizo chini ya kanuni za kisheria na RWAs, yaani mali za ulimwengu halisi.

Habari hii ilisambaa haraka katika ekosistemi. Giovanni Gargiulo, ambaye amekuwa na nafasi muhimu katika kuendeleza na kueleza kazi hii ndani ya Cardano Foundation, aliangazia wachangiaji wengi walioshiriki.

Alimshukuru hasa Phil DiSarro kwa muundo wa mwanzo, pamoja na wakaguzi na wahariri wa CIP. Pongezi pia zinakwenda kwa [Michele Nuzzi] wa Harmonic Labs, aliyekuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuchunguza namna ya kutekeleza programmable tokens kwenye Cardano.

Matteo Coppola, wa FluidTokens, ambaye pia ameshiriki katika kazi hii, na Danny Ribar wa Project Catalyst, waliangazia miaka ya kazi iliyohitajika. Danny alisisitiza changamoto inayofuata: kuifanya itumike.

Adam Dean alieleza kuingizwa kwake kwenye hazina kuu kama hatua nyingine kuelekea hadhi ya Active.
Kwa maelezo ya kiufundi zaidi, kipindi cha Developer Office Hour pamoja na Giovanni kinaeleza CIP-113 na kiwango chake kidogo kinachohusu KYC.

:link: Soma CIP-113 kwenye GitHub.

:link: Fuata majadiliano kuhusu CIP-113 kwenye GitHub..


:desktop_computer: Update ya Cardano Node na ukumbusho wa SPO Call

Intersect imetoa Cardano Node version 11.1.3, update ndogo lakini muhimu kwa SPOs na waendeshaji wa node.

Toleo hili linarekebisha tatizo la kusoma anwani za IPv4 lililoingia katika version 11.1.2, baada ya tatizo kutambuliwa kwenye Preprod testnet.

Intersect inapendekeza SPOs watumie angalau version 11.1.2. Wale ambao bado wanatumia version ya zamani zaidi wanapaswa kwenda moja kwa moja kwenye 11.1.3.

Habari nzuri ni kwamba hakuna haja ya kufanya ledger replay, yaani kusoma na kuchakata upya historia yote ya ledger.

Update hii inalenga kurekebisha tatizo na kuendelea kulinda uthabiti wa mtandao pamoja na utendaji mzuri wa node.

:link: release details na changelog

SPO Call ya wiki hii

Usisahau kujiunga na SPO Call, Alhamisi tarehe 1 Oktoba saa 15:00 UTC.

Mazungumzo yataangazia:

  • Updates za hivi karibuni za core node;

  • Leios na Musashi testnet;

  • Aina tofauti za node, pamoja na Blink Labs na Dingo;

  • Maendeleo ya hivi karibuni kuhusu Mithril.

SPOs wote wanahimizwa kushiriki katika mazungumzo. Kuja na maswali yako!

:link: ongeza SPO Call kwenye kalenda hapa


:globe_showing_asia_australia: Cardano kwenye TOKEN2049: Singapore, tunakuja!

TOKEN2049 Singapore imebaki zaidi kidogo ya wiki moja. Cardano Foundation itashiriki kama Platinum Sponsor, ikiwa na stand ya Cardano ya mita za mraba 108 katika Marina Bay Sands, tarehe 7–8 Oktoba. Tangazo Kamili hapa

Stand ya Cardano itakuwa na miradi 20 iliyochaguliwa kutoka katika ekosistemi. Washiriki watapata nafasi ya kukutana na kuzungumza moja kwa moja na timu zinazojenga miradi hiyo.

Kutakuwa pia na sehemu ya podcast, mawasilisho ya wajenzi na programu kuhusu aina tofauti za node, ikiwemo Node Diversity Celebration Day, tarehe 6 Oktoba.

Tembelea tovuti ya Cardano TOKEN2049 ili kuona programu nzima na miradi itakayowakilisha ekosistemi.

TOKEN2049 Origins Hackathon, matukio ya pembeni kama Rooftop UTXO Pitch Night pamoja na Draper Dragon, na shughuli nyingine zitafanya wiki hiyo iwe na mambo mengi.

Midnight nayo itashiriki ikiwa na programu yake. Tembelea ekosistemi ya Midnight.

Kama ulikosa AMA ya Cardano Foundation kwenye X ya wiki iliyopita, unaweza kuisikiliza kabla ya tukio.


:man_technologist: Developer Spotlight: ODATANO

Katika toleo jipya la Developer Spotlight, Maximilian weber, aliyeunda ODATANO, anaeleza namna uzoefu wake katika kutengeneza mifumo ya SAP na hamu yake ya mifumo iliyogatuliwa vilivyomfikisha kuchunguza uwezo wa Cardano katika biashara.

Mahojiano yanaeleza namna ODATANO inavyotumia OData, kiwango ambacho watengenezaji wa SAP tayari wanakifahamu, ili kurahisisha mawasiliano kati ya mifumo ya biashara na Cardano.

Hii inapunguza ugumu ambao watengenezaji wanakutana nao wakati wa kuunganisha blockchain.

Max pia anaeleza miradi kama TRACE na QUANTIX, akionyesha namna Cardano inaweza kutumika katika:

  • Mnyororo wa usambazaji;

  • Ununuzi wa biashara;

  • Taarifa za kifedha.

Anashiriki maoni yake kuhusu maeneo ambayo Cardano inafaa kwa matumizi ya biashara, mambo yanayohitaji kuboreshwa na kile kinachohitajika ili kuhamisha blockchain kutoka kwenye laptop ya mtengenezaji hadi kwenye mifumo ya biashara inayotumika katika maisha halisi.

:link: Developer sportlight kamili


:clipboard: Updates za Cardano Improvement Proposals — CIP

Kundi lingine la mapendekezo ya CIP limewasili. Lengo kuu ni kuifanya Cardano iwe imara zaidi, iwe rahisi kufuatilia na iwe ya kuaminika zaidi.

Taarifa ya hivi karibuni ya Robert Phair inaleta mapendekezo sita mapya, kuanzia mfumo wa ujumbe unaoweza kusaidia wakati wa dharura hadi vifaa vya kuonyesha vizuri kile node zinafanya.

Pendekezo kubwa lililosubiriwa kwa muda mrefu pia limekamilisha hatua hii.

Mapendekezo mapya

Mapendekezo haya ya CIP na CPS yanahusu mfumo wa kusambaza ujumbe wa kuaminika kwa Cardano. Yanajumuisha chaguo zinazohusu Cardano na intaneti kwa ujumla, pamoja na kufanya kazi nje ya blockchain wakati wa hali za dharura:

Mapendekezo mawili mengine yanahusu uchunguzi wa utendaji katika mtandao wenye aina tofauti za node:

Na mengine mawili:

Linaloendelea kukaguliwa

Lililokamilika


:newspaper: Cardanians: Habari za kila wiki za ekosistemi

Cardanians Newsletter #142, iliyotolewa tarehe 28 Septemba, inaangazia habari kadhaa muhimu kutoka katika ekosistemi.

Charles Hoskinson alieleza smart contracts za faragha na uhamisho wa mali kwa faragha wa Midnight kama hatua kubwa ya kimuundo ikilinganishwa na blockchains za faragha zilizopo.

Newsletter pia inaangazia kuzinduliwa upya kwa soko la NFT la JamOnBread kwenye Cardano.

Vilevile, ukaguzi wa AlphaGrowth kuhusu mifumo ya DeFi umeonyesha mapungufu manane katika mfumo wa sasa wa Cardano DeFi. Haya ni maelezo muhimu kwa mtu anayejenga au kutumia DeFi kwenye blockchain.

:link: mfululizo kamili ya kazi yao hapa


:rolled_up_newspaper: Cardano Newsletter: Weekly Cardano Digest

lucas macchiavelli amerudi na toleo #145, lililotolewa tarehe 28 Septemba.

Linaangazia:

  • Uzinduzi wa Barça Fan Lab;

  • Habari za uhifadhi wa Native Tokens kupitia Fireblocks;

  • Update ya wallet ya Lace 2.3, ambayo imebadilisha namna ya kutafuta stake pools na DReps.

Habari hizi na nyingine nyingi ziko katika Cardano Newsletter ya hivi karibuni.

:link: Soma Weekly Cardano Digest #145 hapa.


:movie_camera: Waundaji wa maudhui ya Cardano wanaangaziwa

Cardano ina watu wengi wanaoandika kuhusu maendeleo yake, wanaoieleza na wanaojenga hadharani. Wiki hii, tunatambua kazi yao na kuwapongeza.

Hapa kuna sauti tofauti: waundaji wa maudhui wanaorahisisha updates za kiufundi na misingi ya staking kwa wanaoanza, pamoja na wajenzi wanaotoa habari moja kwa moja kuhusu kazi wanazofanya.

Peter Bui

Peter Bui, balozi wa Cardano, amechapisha video yenye kichwa “Cardano and Midnight Are Getting More Usable”, yaani Cardano na Midnight zinakuwa rahisi zaidi kutumia.

Video hii ya karibu dakika 35 inakusanya maendeleo makubwa ya wiki:

  • Kuunganishwa kwa Fireblocks;
  • Matumizi ya Cardano kupitia Barça Fan Lab;
  • Update ya Catalyst 2026 Pilot;
  • Habari za Cardano Venture Hub.
    Ni chaguo zuri kama unapenda kupata habari hizi katika maelezo moja yanayofuatana vizuri. :link: ona video hapa

Sadık Emre ALKAN

Mwanajamii Sadık Emre ALKAN ameshiriki maelezo ya kielimu yanayorudi kwenye misingi.
Anaeleza namna Cardano inavyotanguliza utafiti, akiilinganisha na blockchains zinazotanguliza kujenga. Pia anaeleza kwa nini muundo wa zero-knowledge wa Midnight unafuata msimamo huo huo.
Ni makala ndefu kidogo, lakini yenye manufaa kwa mtu anayependa kuelewa falsafa inayoongoza muundo wa mfumo. Soma Hapa x post yake


:books: Mafunzo kwa jamii na ushiriki wa watengenezaji

Kipindi cha Developers Office Hour kilichotolewa tarehe 28 Septemba kilikuwa na Dominic Wallis, Senior Software Engineer katika Cardano Foundation.

Aliwasilisha Subbit.Xyz, mfumo mwepesi wa njia za malipo za Layer 2, unaowezesha malipo ya usajili na malipo madogo bila kutegemea uaminifu kwa mtu wa kati.

Kipindi hiki kinatoa mfano wa vitendo unaokamilisha maendeleo ya malipo ya mawakala wa AI kupitia x402 katika ekosistemi ya Cardano.

Hydra Technical Workshop

Hydra Technial Workshop itaeleza: * Mfumo wa state channels wa Hydra; * Mifano ya matumizi katika programu;

  • Hatua za kuandaa mfumo wa kiufundi; * Maswali na majibu moja kwa moja pamoja na timu ya Hydra.
    Watengenezaji wanaopenda programu za Layer 2 zenye uwezo mkubwa wa kuchakata miamala kwenye Cardano wanahimizwa kushiriki.

Kumbusho kuhusu tarehe: Makala ya asili inataja tarehe 2 Oktoba saa 14:00 UTC katika sehemu hii, lakini orodha ya matukio inataja 1 Oktoba saa 14:00 UTC. Tafadhali angalia link ya tukio ili kuthibitisha tarehe.

Usalama wa smart contracts wakati wa maendeleo ya AI

Tarehe 28 Septemba, kipindi cha Roundtable Talk: Smart Contract Security — Why One Check Is No Longer Enough kilikusanya wataalamu wenye uzoefu wa usalama.

Walichunguza namna maendeleo ya haraka ya AI yanavyobadilisha usalama wa smart contracts.

Mazungumzo yaliangazia namna mifumo ya AI sasa inaweza kuchambua code, kutambua mapungufu ya usalama na kutengeneza code ya kuyatumia katika dakika chache.

Hii inaleta maswali mapya kuhusu:

  • Ufuatiliaji unaoendelea;

  • Nafasi ya ukaguzi wa kawaida;

  • Uaminifu katika ekosistemi.

Wataalamu pia walizungumzia namna kampuni za ukaguzi zinavyobadilisha mifumo yao ya biashara, na hatua ambazo watengenezaji wa DApps wanaweza kuchukua ili kuimarisha usalama na kulinda watumiaji.

Washiriki walikuwa:


:classical_building: Habari kutoka Cardano Foundation

Cardano Foundation imeendelea na shughuli zinazohusu elimu, matumizi katika maisha halisi, uchumi wa mawakala wa AI kupitia x402, na utawala.

Ushirikiano na UCLA

Tarehe 28 Septemba, Foundation ilitangaza ushirikiano wa miaka kadhaa na Venture Accelerator ya UCLA Anderson School of Management. zaidi uta pata hapa

Ushirikiano huu unajumuisha:

  • Nafasi tano za fellowship zinazofadhiliwa kwa kampuni changa katika programu ya UCLA Accelerate;

  • Masterclass ya blockchain na AI yenye ushiriki wa moja kwa moja, tarehe 19 Oktoba, yenye kichwa “Cardano for the Real World”;

  • Kuingizwa kwa maudhui ya Cardano Academy katika masomo ya blockchain ya UCLA Anderson kuanzia 2027;

  • Ufadhili wa UCLA Draper Innovation Showcase 2027.

:link: maelezo ya ushirikiano kwenye crypto.news

Barça Fan Lab kwenye Cardano

FC Barcelona ilizindua rasmi Barça Fan Lab, tarehe 25 Septemba.

Jukwaa hili limefadhiliwa kupitia Catalyst Fund 13 na kujengwa kwa ushirikiano na Andamio. Linaunganisha utambulisho wa kidijitali wa mashabiki wa BarçaID na wallet ya Cardano Web3.

Hii inafungua njia ya kutumia:

  • Vyeti vinavyoweza kuthibitishwa;

  • Badges za elimu;

  • Tokeni za kupata huduma au nafasi fulani;

  • Vitu vya kidijitali vya kukusanya.

Washiriki hawahitaji kuwa na ujuzi wa juu wa blockchain.

Cardano kwenye SDK rasmi ya x402

Foundation imethibitisha kwamba Cardano sasa inapatikana kwenye SDK rasmi ya x402.

Wahandisi wa Foundation wamechangia sehemu za client, server na facilitator, zinazowezesha malipo ya API kwa ada kutoka kwa mawakala wa AI na programu.

Hii inaingiza Cardano katika mpango mpana wa x402 unaoendelezwa na Coinbase, unaolenga malipo kati ya mashine kupitia HTTP ya kawaida.

:link: Cardano kwenye SDK rasmi ya x402

Takwimu za miaka 9 ya Cardano

Kwa maadhimisho ya tarehe 23 Septemba, Foundation ilishiriki takwimu hizi:

  • Ada bilioni 38.89 zinazozunguka;

  • Ada bilioni 21.29 zilizowekwa kwenye staking;

  • Stake pools hai 2,672;

  • DReps hai 328;

  • Hatua 158 za utawala tangu kuanza kwa kipindi cha Voltaire.

:link: soma mengi hapa

UNDP SDG Blockchain Accelerator

Kipindi cha kutuma maombi kwa UNDP SDG Blockchain Accelerator kinaingia wiki yake ya mwisho.

Timu za Umoja wa Mataifa zinaalikwa kuwasilisha changamoto za maisha halisi ambazo teknolojia ya blockchain inaweza kusaidia kutatua.

:link: *UNDP SDG Blockchain Accelerator

“What’s next for Cardano?”

Tarehe 22 Septemba, X Space iliyoandaliwa na Foundation ilileta pamoja CEO Frederik Gregaard, wachangiaji kutoka timu ya node mbadala ya Amaru, na jamii.

Mazungumzo yaliangazia muundo wa Catalyst 2026 Pilot na mipango ya matukio ya jamii kwa mwaka 2027.

:link: Mengi Utapata hapa


:handshake: Habari kutoka Intersect MBO

Matokeo ya uchaguzi wa Board 2026

Intersect ilitangaza matokeo ya uchaguzi wake wa Board tarehe 28 Septemba.

Adam Rusch na Kavinda Kariyapperuma walichaguliwa kutoka miongoni mwa wagombea 11. Wanachama 139 wa Intersect walipiga kura.

Intersect iliwashukuru pia wagombea tisa ambao hawakuchaguliwa na kuwahimiza waendelee kushiriki kupitia kamati na vikundi vya kazi.

Intersect Weekly Update #130

Intersect Weekly Update #130, iliyochapishwa tarehe 26 Septemba, iliangazia maendeleo ya utawala na teknolojia.

Civics Committee imekamilisha kuboresha sehemu yake ya taarifa na nyaraka. Imepanga upya nyaraka za utawala na kuongeza kurasa kuhusu:

  • Kupunguzwa kwa viti vya Constitutional Committee hadi vitano;

  • Ushauri wa jamii duniani kuhusu Katiba;

  • Uchaguzi wa Constitutional Committee wa 2026.

Kwa upande wa teknolojia, Node Development Roadmap inaonyesha kwamba Node 11.2 inatarajiwa kuleta uwezo wa kwanza wa kipindi cha Dijkstra, ukiwemo Plutus V4.

Parameter Committee pia inachunguza karibu masharti 150 ya ulinzi yanayohusu Dijkstra na Peras kwa pamoja. Intersect news page.

Kura zinazokaribia tarehe ya mwisho

Hatua kadhaa za utawala kwenye blockchain zinakaribia mwisho wa muda wake tarehe 11 Oktoba, zikiwemo:

  • Ombi la kutoa fedha kutoka hazina kwa OpenZeppelin Stack;

  • Pendekezo la kupunguza minPoolCost hadi ADA 75;

  • Kura ya maoni kuhusu k-parameter, inayoweka lengo la idadi ya stake pools.

DReps na SPOs wanahimizwa kuchunguza mapendekezo haya na kupiga kura kabla ya tarehe ya mwisho.
Vipindi vya Governance Hour pamoja na Nicolas Gerny vinatoa maelezo ya kina kuhusu OpenZeppelinna pendekezo la kupunguza minPoolCost hadi ADA 75. Reduce minPoolCost to 75 ADA (

Constitutional Amendment Portal — CAP

CAP bado iko wazi kwa ushauri wa jamii, ikiwa na mapendekezo saba yanayochunguzwa.

CAP-3: Net Change Limit Strategic Spending Plan imepata ushiriki mkubwa zaidi mpaka sasa, ikiwa na maoni 18 kutoka kwa jamii.

Sasa inawezekana kuunganisha wallet. Kipindi kinachofuata cha ukaguzi wa CAP kimepangwa tarehe 1 Oktoba saa 14:00 UTC.
Constitutional Amendment Portal (CAP)


:magnifying_glass_tilted_right: Mada 10 za Cardano Forum zilizotembelewa zaidi kupitia vyanzo vya nje

Hizi ni mada zilizopata mibofyo mingi zaidi kutoka kwenye vyanzo vya nje katika siku 10 zilizopita:

  1. Cardano Summit 2026 + TOKEN2049: Treasury Proposal FAQ
    Maswali yanayoulizwa mara nyingi kuhusu pendekezo la hazina.

  2. Intersect 2026 Elections: Open Forum for Candidate Presentations and Community Questions
    Jukwaa wazi la mawasilisho ya wagombea na maswali ya jamii.

  3. *Why I’m Running for Intersect in 2026 & The Candidates I Voted For*
    Kwa nini ninagombea Intersect mwaka 2026 na wagombea niliowapigia kura.

  4. Constitutional Committee Result: New Heights
    Matokeo ya Constitutional Committee: New Heights.

  5. Cardano Foundation Voting Decisions: 2026 Intersect Budget Process
    Maamuzi ya kura ya Cardano Foundation kuhusu mchakato wa bajeti ya Intersect wa 2026.

  6. Digest September 02, 2026: Intersect Board Elections, CAP, Daedalus 11.3.0, and more
    Digest ya tarehe 2 Septemba 2026.

  7. Governance Hour #5 — IO Consensus Initiative Proposal
    Pendekezo la IO Consensus Initiative.

  8. Cardano Ecosystem Update | Van Rossem, Leios, Midnight and the Road Ahead
    Habari za ekosistemi: Van Rossem, Leios, Midnight na hatua zinazofuata.

  9. Security Blind Spot — Ecosystem Security as a Shared Responsibility
    Mapungufu yasiyoonekana ya usalama: usalama wa ekosistemi kama wajibu wa pamoja.

  10. Attending the Linux Foundation Open Source Summit: People Are Ready for Blockchain
    Kushiriki Linux Foundation Open Source Summit: watu wako tayari kwa blockchain.


:date: Matukio yajayo ya jamii

30 Septemba — Q3 Intersect Insight na DRep Monthly Call

DReps wanakutana kuchunguza maendeleo ya utawala na kura zinazokuja.

:link: Mikutano mbali mbali

1 Oktoba — CAP Review Session

Saa 14:00 UTC. Raundi inayofuata ya ushauri wa jamii kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya Katiba yanayoendelea.

:link: Cap Review session

Hydra Technical Workshop — Developers Office Hours #80

Kipindi cha maelezo ya kina kuhusu mfumo wa state channels wa Layer 2 wa Cardano, pamoja na maswali na majibu moja kwa moja.

Saa 14:00 UTC. Makala ya asili inataja tarehe 1 Oktoba katika orodha ya matukio na 2 Oktoba katika sehemu ya mafunzo. Angalia link rasmi ili kuthibitisha tarehe.

:link: Hydra Technical Workshop

6 Oktoba — Hard Fork Working Group

Mkutano wa mtandaoni kwa watengenezaji wanaofuatilia mchakato wa update ya Dijkstra. Angalia ukurasa wa Luma ili kuthibitisha tarehe.

:link: Hard Fork Working Group kwenye Luma

6–8 Oktoba — Cardano Singapore

Cardano Node Diversity Celebration na programu ya Cardano Summit 2026 zitafanyika Singapore, pamoja na TOKEN2049, mojawapo ya mikutano mikubwa ya blockchain na mali za kidijitali katika eneo la Asia-Pacific.

:link: ya programu ya Cardano Singapore

Kwa matukio mengine ya kila wiki, tembelea Cardano Events.

:link: Cardano events, mikutano zengine


Tafsiri ya Kiswahili imeandaliwa na Olivier Rishi Matabaro Olivier RISHI,Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ili kusaidia jamii inayozungumza Kiswahili kufuatilia habari za Cardano.

Chanzo: Cardano Community Digest — 30 Septemba 2026.